31 Mei 2014 - 07:28
Mutharika achukua kiti cha urais Malawi

Baada ya mivutano ya kisheria kwa wiki nzima hatimaye Peter Mutharika atambulishwa kama rais mpya wa Mawali.

Profesa Peter Mutharika aliyegombea kwa tiketi ya chama cha DPP ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 36.4 ya kura zote akifuatiwa na Dr Lazarus Chakwera mwenye asilimia 27.8 huku Rais anayemaliza muda wake Dr Joyce Banda akishika nafasi ya tatu kwa asilimia 20.2 na Atupele Muluzi amekuwa wa nne na asilimia 13.7
Uchaguzi wa Malawi ulifanyika Mei 20 nchini kote lakini mara tu baada ya kumalizika zoezi la upigaji kura, kulizuka migogoro na mashataka mengi kuhusu uchaguzi na malalamiko yakafikishwa mahakama kuu za Lilongwe na Blantyre.